Chuo kikuu Alkafeel kimeandaa semina ya utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanafunzi wake

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel kimeandaa semina inayohusu utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanafunzi wake.

Semina hiyo inasimamiwa na idara ya mafunzo na elimu endelevu katika chuo kwa kushirikiana na wakufunzi wa Alkafeel katika mambo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza ili kujenga uwezo wa wanafunzi katika kupambana na majanga.

Semina hiyo inawakufunzi wawili ambao ni Amiri Rashidi Hadadi na Sefu Abbasi Kadhim, wamefundisha mambo mbalimbali kwa nadhariyya na vitendo.

  • - Ratiba ya kwanza inaitwa (Katika kila nyumba muokozi), inahusisha namna ya kusaidia mtu mwenye matatizo ya moyo kwa wazee na watoto.
  • - Ratiba ya pili inaitwa (Huduma ya kwanza), inahusisha utoaji wa huduma ya kwanza kwa mtu aliyevunjika mfupa, matukio ya moto na mambo mengine anayoweza kukumbana nayo Zaairu.

Mwisho wa semina washiriki hupewa mtihani, kwa ajili ya kupima uwelewa wao katika masomo waliyo fundishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: