Atabatu Abbasiyya tukufu yaomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)

Maoni katika picha
Ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kilicho tokea mwezi ishirini na tano Muharam.

Kiongozi wa idara ya wahadhiri Shekhe Abduswahibu Twaaiy amesema: “Majlisi ya kuomboleza hufanywa kila mwaka, na huzungumzwa historia ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s), majlisi itadumu kwa muda wa siku tano kuanzia siku ya Jumamosi (21 Muharam)”.

Akaongeza: “Majlisi huwa na mihadhara miwili, mhadhara wa kwanza hutolewa baada ya swala ya Dhuhuraini na Shekhe Ali Saaidiy, na wa pili hutolewa jioni na Sayyid Ihsani Alhakiim Mula na Haidari Swaghiru Alkadhimiy”.

Akafafanua kuwa: “Mada zinazo zungumzwa zinahusu historia ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s), na mtihani mkubwa aliopitia pale aliposhuhudia mauwaji ya Twafu na kifo cha baba yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), na jinsi alivyo salimika katika mauaji hayo kwa hekima ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ili aendeleze safari ya baba yake Hussein (a.s) ya kupambana na matwaghuti na kufundisha uislamu halisi”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika yameongelewa mafanikio aliyopata Imamu Sajjaad (a.s), kutokana na umadhubuti wake, elimu na uchamungu, na jinsi alivyotumia Maisha yake katika kufanikisha malengo ya Imamu Hussein na kupambana na njama za bani Umayya, sambamba na kuongea mazingira ya kifo chake mwishoni mwa kila majlisi”.

Kumbuka kuwa majlisi hizi hufanywa kila mwaka chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) wa kuhuisha matukio yanayohusu Maimamu wa Ahlulbait (a.s), likiwemo tukio hili tunalo zungumzia siku hizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: