Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa warsha yenye anuani isemayo (Mkakati wa kusoma harakati) kwa watumishi wa kitengo cha malezi katika mkoa wa Dhiqaar.
Mkufunzi wa warsha hiyo bwana Farasi Shimri amesema: “Warsha imefanyika kwa muda wa siku mbili, kila siku wamekaa darasani saa tano na kusoma mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uwelewa wa kusoma harakati na matumizi yake”, akabainisha kuwa “Washiriki wametoa ushirikiano mkubwa, ukizingatia ugeni wa taaluma na uwezekano wa kuifanyia kazi kwa vitendo katika mazingira ya malezi na ufundishaji”.
Washiriki wametoa shukrani kwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kujali sekta ya malezi.
Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kuratibu warsha na semina za kielimu, zinazolenga kuboresha uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu katika mambo mbalimbali.