Atabatu Abbasiyya tukufu imesema: Ziara ya Arubaini imekua ziara ya kitaifa

Maoni katika picha
Ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Afdhalu Shami amesema kuwa, ziara ya Arubaini imekua ziara ya kitaifa hapa Iraq, inamambo mengi yanayohusu taifa hili na raia wake.

Ameyasema hayo katika ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumanne kwenye warsha ya vituo vya kuelekeza wasafiri.

Akaongeza: “Ni wazi kuwa miongoni mwa ziara kubwa za Imamu Hussein (a.s) ni ziara ya Arubaini, baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa ni miongoni mwa alama za Imani tano zilizo tajwa katika hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imamu Askariy (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Hii sio ziara ya Dini tu, kwani inamambo mengi yanayohusu taifa hili na raia wake, japokua ni ziara ya kidini lakini pia ni ziara ya kitaifa”.

Akabainisha kuwa: “Idadi kubwa za watu huja Karbala kutoka ndani na nje ya Iraq, na jinsi raia wa Iraq wa tabaka zote wanavyo wapokea na kuwahudumia, inaonyesha wazi kuwa hii ni ziara ya kitaifa, ni muhimu kuangaziwa na vyombo mbalimbali vya Habari, hata kama kikiwa sio chombo cha Dini kinaweza kuripoti ziara hii kwani inahusisha taifa kwa kiwango kikubwa”.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria akasema: “Kuna zaidi ya aina (50) ya huduma zinazotolewa kwa mazuwaru, miongoni mwa huduma hizo ni chakula, tiba na zinginezo, ikiwemo huduma ya kurudisha waliopotea kwa jamaa zao, huduma hii ni muhimu sana kibinaadamu, watoaji wa huduma hiyo wanapata thawamu mbele ya Mwenyezi Mungu”.

Akafafanua kuwa: “Zamani tulikua na kituo kimoja cha kurudisha waliopotea kwa jamaa zao, mwaka (2004), kisha baadae vikaongezeka na kuwa vine, hadi sasa vimekua vingi sawa na idadi ya nguzo za barabarani, sambamba na kuwa na ushirikiano wa vituo mbalimbali vya Karbala na Najafu, kisha umefanyika uboreshaji wa kimtandao kwa kiwango kikubwa hadi sasa kuna vitengo vingi vinavyo shiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: