Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanahuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya Jumatano (25 Muharam 1444h), watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Matembezi hayo yameanzia ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wanaimba kaswida za kuomboleza.

Matembezi yakaishia ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza iliyo hudhuriwa na watumishi wa Ataba mbili na kundi la mazuwaru.

Kumbuka kuwa watumishi wa Ataba mbili tukufu katika mji wa Karbala, hufanya matembezi rasmi ya kuomboleza katika kila kumbukumbu ya kifo cha Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: