Wanahabari wa Atabatu Abbasiyya wanashiriki kwenye warsha ya kamati ya Habari na mawasiliano

Maoni katika picha
Kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya kimeshiriki kwenye warsha ya utambulisho, iliyo andaliwa na kamati ya Habari na mawasiliano katika mji wa Karbala.

Kiongozi wa kitengo cha Habari na mahusiano katika kamati ya Habari na mawasiliano Sayyid Ammaari Mahmuud amesema “Warsha ya leo inahusu kuangazia uvumi uliopo kwenye sekta ya Habari na kufanya uhakiki kabla ya kuzitoa, sambamba na kutambulisha kanuni za urushaji wa Habari kwenye luninga, zinazohusu kamati ya Habari na mawasiliano”.

Akaongeza kuwa “Warsha imepata muitikio mkubwa kutoka kwa vyombo vyote vya Habari katika mkoa wa Karbala na Ataba tukufu”, akabainisha kuwa “Mhadhiri wa warsha hiyo alikua ni Profera Kaamil Qiyam kutoka mji wa Hillah”.

Kiongozi wa Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Jasim Saidi amesema “Ushiriki wa Ataba kwenye nadwa na warsha hizi ni muhimu sana, kwani zina mitandao ya kijamii”, akaongeza kuwa “Tunahitaji kuwa na warsha kama hizi kwa ajili ya kujifunza namna ya kulinda mitandao ya Ataba tukufu, hakika kutambua kanuni za kamati ya Habari na mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa taasisi yeyote ya Habari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: