Wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu wanafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)

Maoni katika picha
Wanafunzi wa tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mjini Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina Sajjaad (a.s).

Kiongozi wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema “Lengo la kufanya majlisi hii ni kutoa elimu ya Dini na kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya na kuhamasisha wanafunzi kuendelea kufanya hivyo siku zijazo”.

Kiongozi wa idara ya tahfiidh katika Maahadi Abdulhamidi Swaghiru amesema: “Wanafunzi wa kitengo cha Tahfiidh wanafanya majlisi hii kwa mwaka wa pili mfululizo, akabainisha kuwa majlisi hii inafanywa sambamba na maombolezo ya Ashura kwa muda wa siku tatu kuanzia leo”.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Muhammad Hassan Nizaar na sehemu ya Nai ya mwanafunzi Mahadi Muhammad Raatibu kisha majlisi iliyosomwa na Shekhe Qassim Janabi na kuhitimishwa kwa kaswida iliyosomwa na Amiri Najafiy.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: