Atabatu Abbasiyya inatoa rambirambi kwa majeruhi wa ajali ya treni

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa rambirambi kwa familia za wahanga wa ajali ya Treni kwa watu wa mkoa wa Basra.

Ugeni umetoa pole za dhati kwa wahanga hao na kusisitiza kuwa ajali hiyo imeumiza roho za raia wote wa Iraq, na sio familia za wahanga peke yake.

Yamesemwa hayo walipo tembelea familia iliyopoteza watu watatu kwenye ajali hiyo mbaya ya Treni katika mji wa Basra.

Watu wa Basra wameshukuru sana watu wote walio saidia kuokoa wahanga wa ajali, Pamoja na msaada mkubwa uliotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa vikosi vya uokoaji.

Ugeni huo umezawadia familia hiyo bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu -toka dakika ya kwanza- ilituma wahandisi na misaada ya kibinaadamu kwa vikosi vya uokozi, sambamba na kuwasiliana na familia zilizofiwa kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli za mazishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: