Maahadi ya Qur’ani tukufu inafanya mitihani ya nadhariyya kwa wanafunzi wake katika hukumu za usomaji

Maoni katika picha
Idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya mitihani ya nadhariyya kwa wanafunzi wa semina ya hukumu za usomaji.

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Watahiniwa wapo ishirini, wamesomeshwa hukumu za usomaji kwa muda wa miezi mitatu, kila wiki walikua wanasoma mada mbili chini ya ukufunzi wa Sayyid Dhulfiqaar Saaburi”, akasema: “Wanafunzi hao wanapenda sana Qur’ani na wanatoka tabaka tofauti za jamii”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu huendesha semina mbalimbali za Qur’ani katika kipindi cha mwaka mzima, kwa lengo la kupanua wigo wa Qur’ani katika jamii, kupitia semina hizo tumefanikiwa kufaulisha mamia ya walimu na wanafunzi wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: