Kitendo cha Dini kinaendelea na semina zake kwa watumishi

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendelea kufanya semina za kuwajengea uwezo watumishi katika mambo ya Fiqhi, Aqida na Akhlaqi.

Sayyid Muhammad Mussawi kutoka idara ya Tablighi ya kidini amesema: “Kitengo cha Dini kilianza kufanya semina kwenye zaidi ya sekta 20 za kielimu sambamba na kusaidia harakati za Tablighi kwa lengo la kuboresha uwezo wa watumishi”.

Akaongeza kuwa: “Kuna ratiba maalum ya kuwajenga watumishi kwa kuwapa semina, ukizingatia kuwa wapo karibu na mazuwaru, hakika semina hizi zimekua na matokea mazuri”.

Akasema: “Semina zinaendelea kwa vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu vipatavyo (36), semina zipo za aina mbili, kuna semina maalum kwa watumishi wapya na semina za watumishi wa zamani, hufundishwa mambo ya Fiqhi, Aqida, Akhlaqi kwa muda wa siku 15, kila mwisho wa semina washiriki hupewa mtihani”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya semina mbalimbali zinazo lenga kuwajenga watumishi wake kwenye mambo tofauti ya kidini na kitamaduni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: