Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa pole kwa familia ya Aali-Hakiim katika mkoa wa Najafu, kwenye hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza tangu alipofariki Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Hakiim.
Ugeni wa Atabatu Abbasiyya umeongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, ameongozana na katibu mkuu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Afdhalu Shami amesema: “Tupo katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza tangu alipofariki Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Hakiim (q.s), Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini, baadhi ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi wanatoa pole sana kwa familia tukufu ya Aalu-Hakiim”.
Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Hakiim (q.s), aliyetumia umri wake katika kutafuta elimu na kuifundisha pamoja na kuhudumia uislamu na waislamu, alikufa siku ya Ijumaa mwezi ishirini na tano Muharam mwaka jana, kwa maradhi ya moyo, jeneza lake lilishindikizwa na watu wengi sana katika mji wa Karbala na Najafu.