Chuo kikuu Al-Ameed kinajiandaa kutoa jarida la kwanza la kielimu

Maoni katika picha
Chuo kikuu Al-Ameed kinajiandaa kutoa jarida la kwanza la kielimu liitwalo: (Al-Ameed Journal for Medical Research and Health Sciences), linalenga kusambaza tafiti za kielimu kwa walimu na wanafunzi wa ndani na nje ya Iraq.

Rais wa chuo cha Al-Ameed Dokta Muayyad Alghazali amesema: “Chuo kitafanya semina na timu ya Daru-Safiir ya usambazaji wa Makala za kielimu, kwa lengo la kukamilisha vipengele vya kazi hiyo na kanuni muhimu za chuo”.

Akasisitiza kuwa “Jarida hili linaumuhimu mkubwa katika kusambaza elimu za kitafiti na kuziendeleza, elimu ambazo ni msingi wa maendeleo ya kitaasisi na kivyuo”.

Akaongeza kuwa “Watafiti wanaweza kuandika tafiti zao kwenye toleo hilo, waandae tafiti zao na kuzituma kwenye link maalum ya jarida, itakayo wekwa kwenye mtandao wa chuo siku ya tangazo la jarida”.

Akasema: “Tangazo la jarida litatolewa siku ya tarehe (24/11/2022m), ambayo ni siku ya majarida na kumbukumbu ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Al-Ameed”, akasisitiza kuwa: “Kutakua na majarida mengi, jarida la tiba, famasiya, tiba ya meno na uuguzi, majarida hayo yanamchango mkubwa wa kutoa elimu na kushajihisha watafiti katika taifa letu”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya kazi kubwa ya kuboresha sekta ya elimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: