Ugeni kutoka wizara ya kilimo umetembelea Atabatu Abbasiyya na kujadili njia za kuboresha sekta ya kilimo

Maoni katika picha
Ugeni kutoka wizara ya kilimo umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Jumamosi, na kujadili njia za kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini.

Ugeni huo ulikua na watafiti wa kilimo walio ongozwa na rais wao Dokta Farasi Muzahimu.

Wamepokewa na rais wa kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ali Azharu, na mkuu wa mawasiliano na mauzo katika shirika la Khairul-Juud Sayyid Falahu Fatliy.

Wamejadili umuhimu wa kuboresha sekta ya kilimo hapa Iraq.

Aidha ugeni huo umepewa maelezo kuhusu miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sambamba na kuonyesha harakati zinazofanywa na shirika la Khairul-Juud katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa pembejeo za kilimo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: