Kuanza hatua ya kwanza ya matembezi ya wapenzi wa Husseini

Maoni katika picha
Wilaya ya Fau katika mkoa wa Basra leo siku ya Jumamosi, imeshuhudia msafara wa kwanza kuelekea Karbala kwa ajili ya kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Msafara huo ni sawa na tangazo la kuanza kwa matembezi ya Kwenda Karbala, na katika kitongoji cha Ra-asubishah limefanywa kongamano la (Kutoka baharini hadi mtoni) kwa mwaka wa kumi mfululizo, ambalo huratibiwa na taasisi ya maadhimisho chini ya ofisi ya Marjaa Dini Marehemu Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Hakiim (q.s), kwa kushirikiana na vikundi na mawakibu Husseiniyya za Basra, pamoja na serikali na wakazi wa mji wa Fau.

Kongamano limehudhuriwa na viongozi wengi wa Dini na kundi la mazuwaru wanaotarajiwa kutembea kilometa (675) kutoka Basra hadi Karbala.

Mji wa Ra-asushibah katika mkoa wa Basra upo mbali zaidi kusini mwa Iraq, mazuwaru huanza kutembea katika mji huo kila mwaka hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala, kufanya ziara ya Arubaini mwezi ishirini Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: