Idara ya Qur’ani imehitimisha program ya (Ulizeni wanaojua) katika mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani imehitimisha program ya (Ulizeni wanaojua) katika mwezi wa Muharam.

Kiongozi wa program hiyo ambayo ipo chini ya idara ya maelekezo ya kidini upande wa wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, bibi Fatuma Mussawi amesema: “Kuhitimisha ratiba ya program ya (Ulizeni wanaojua) iliyofanywa ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), na kuhudhuriwa na kundi la mazuwaru wa haram takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kundi la wanafunzi wa shule ya Fadak-Zaharaa (a.s) ya Qur’ani kwa wasichana”.

Akaongeza kuwa: “Hafla ya kufunga program imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kutoka juzu la kumi na moja kwa kufuata utaratibu wa kila wiki -Jambo hilo linaonyesha jinsi idara ya Qur’ani inavyo jali Qur’ani tukufu wakati wote, inafundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru, kupitia wasomaji wa idara”.

Akaendelea kusema “Kisha wahudhuriaji wakaenda kufanya ziara kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja, hafafu wakafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s), mzungumzaji akaeleza historia yake tukufu, ukafuata mhadhara wa kifiqhi uliotolewa na mmoja wa wajumbe wa idara ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake”.

Akafafanua kuwa: “Program haikuwa ya wanawake peke yao, bali vijana wadogo walipewa nafasi, walifanyiwa warsha na kuelezwa umuhimu wa kufikisha taarifa sahihi, kwa njia zinazo endana na umri wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: