Atabatu Abbasiyya tukufu inakabidhi bendera ya Imamu Hassan (a.s) kwa Atabatu Askariyya

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umekabidhi bendera ya uombolezaji wa Imamu Hassan (a.s) kwa uongozi wa Atabatu Askariyya, kupitia ugeni rasmi unao ongozwa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami.

Wakati wa kukabidhi bendera kwa uongozi wa Atabatu Askariyya hiyo wito wa kuhudhuria kongamano la tisa la Imamu Hassan (a.s) umetolewa, kongamano hilo litasimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Baabil.

Pande mbili hizo zimejadili njia za kushirikiana Ataba mbili katika sekta tofauti hasa kwenye kuhudumia mazuwaru.

Atabatu Abbasiyya tukufu imekabidhi bendera ya kuomboleza Imamu Hassan (a.s), itakayo pandishwa siku ya kumbukizi ya kifo chake mwezi saba Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: