Jengo la Shekhe Kuleini limejiandaa kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Watumishi wa jengo la Shekhe Kuleini wamejiandaa kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kwa kutoa huduma tofauti.

Kiongozi wa jengo hilo Ali Mahadi Abbasi amesema “Watumishi wa jengo hili wamejiandaa kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubaini”.

Jengo la Shekhe Kuleini lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu umbali wa kilometa 17 kutoka makao makuu ya mji wa Karbala upande wa Bagdad, hupokea maelfu ya mazuwaru wakiwemo na wahudumu wa afya, hutoa huduma kwa zaidi ya watu laki tano, aidha tumeandaa sehemu kadhaa za kutolea huduma za afya.

Akaendelea kusema: “Tunafanya kazi kubwa ya kupunguza joto kwa kutumia vifaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kufunga makumi ya feni”, akasema “Tumeweka mtambo wa kupoza maji safi ya kunywa wenye uwezo wa kupoza lita elfu 10”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: