Markazi Dirasaati Afriqiyya imeweka utaratibu maalum kwa mazuwaru wa kiafrika

Maoni katika picha
Markazi Dirasaati Afriqiyya imeweka utaratibu maalum wa kuhudumia mazuwaru wanaokuja kutoka bara la Afrika wakati wa ziara ya Arubaini.

Markazi Dirasaati Afriqiyya inajukumu la kufanya Tablighi katika bara la Afrika, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa Markazi hiyo Shekhe Saadi Shimri amesema: “Markazi Dirasaati imeweka utaratibu maalum kwa kushirikiana na kituo cha kuelekeza waliopotea, watatoa huduma kwa mazuwaru wa kiafrika”.

Raisi wa kituo cha kuelekeza waliopotea Sayyid Husaam Muhyi-Dini amesema: “Tumeweka utaratibu wa kumuongoza zaairu kwa lugha ya kiengereza kwa ajili ya mazuwaru wa bara la Afrika”.

Shimri akasisitiza kuwa “Kutakua na utaratibu kamilia wa kusaidia mazuwaru katika miji miwili Najafu na Karbala hususan wanaotoka bara la Afrika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: