Kituo cha kuchapisha Qur’ani tukufu kimemaliza kuchapisha chapa mpya ya msahafu mtukufu

Maoni katika picha
Kituo cha kuchapisha Qur’ani tukufu kimekamilisha uchapishaji wa nakala mpya ya Qur’ani yenye wasifu tofauti na nakala iliyotangulia, nakala hii imeandikwa kwa mikono ya raia wa Iraq.

Mkuu wa kituo hicho Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema “Atabatu Abbasiyya ilichapisha nakala ya kwanza ya Qur’ani hapa Iraq, iliyosanifiwa na raia wa Iraq na kuchapishwa hapa nchini, kituo kinaendelea na mkakati wa kuchapisha naka mpya yenye maandishi makubwa, tofauti na zilizopo hivi sasa”.

Akabainisha kuwa “Nakala ya mwaka huu alama zake ziko wazi zaidi na herufi zinamuonekano mzuri nalo ni toleo la sita”.

Akasema “Tunajipanga kuchapisha toleo la saba litakalo kuwa bayana zaidi, linatarajiwa kutoka mwaka 2023m Insha-Allah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: