Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imeandaa mitihani ya majaribio kwa walimu wake, inalenga kuangalia viwango vyao na kuweka mikakati ya kuwaendeleza.
Kiongozi wa Maahadi Sayyidah Manaar Jaburi amesema: “Mitihani ya majaribio ni muhimu katika Maahadi, inatusaidia kutambua uwezo wa walimu wetu wanaofundisha makao makuu ya Maahadi na kwenye tawi la mkoani Najafu”.
Akaongeza kuwa “Mtihani ulikua na maswali mbalimbali yanayo husu kazi zao na changamoto zake, kisha inasahihishwa na kutuwezesha kutambua viwango vyao, halafu tunaandaa semina za kuwajengea uwezo kama ikihitajika”.