Kujiandaa na ziara ya Arubaini.. jengo jipya la kutoa huduma kwa wanawake litaanza kutumika siku chache zijazo

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi kimetangaza kukaribia kuanza kutumika jengo jipya lililojengwa rasmi kwa ajili ya wanawake kwenye barabara ya Najafu – Karbala, wakati wa ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Amidi Swaaighi amesema: “Jengo jipya la wanawake lililopo upande wa mgahawa wa nje wa Ataba tukufu kwenye barabara ya Najafu – Karbala litaanza kutumika katika siku za ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Shirika la Liwaaul-Alamiyya limeahidi kukamilisha ujenzi huo ndani ya muda mfupi, wanafanya kazi kwa zamu tatu kila siku ili waweze kukamilisha ndani ya siku chane zijazo”.

Akabainisha kuwa “Eneo la majengo hayo linaukubwa wa dunam (10), kuna sehemu ya kupumzika mazuwaru, sehemu za kulala watumishi wa kujitolea wakike, kumbi za kutolea huduma za afya, majiko, mtambo wa kusafisha maji, mtambo wa kutengeneza barafu na kituo cha umeme”.

Akasisitiza kuwa “Sehemu zote zimefungwa kamera, vipaza sauti na mitambo ya ulinzi, aidha kuna zaidi ya vyoo (200)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: