Kufanikiwa kwa upasuaji wa uso (Complex process) katika hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa upasuaji wa uso katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyekua na tatizo kwenye uso wake.

Daktari bingwa wa upasuaji wa uso Dokta Ridhwani Twaiy amesema: “Tumemfanyia upasuaji wa uso wenye mafanikio kijana mwenye umri wa miaka 18”.

Akaongeza kuwa “Upasuaji huu ulikua mkubwa kwani tumerekebisha mfupa wa uso, pua, fuvu la kichwa na taya”.

Akasema: “Upasuaji wa aina hii hufanywa katika kituo cha upasuaji wa uso katika hospitali ya rufaa Alkafeel, kwa msaada wa vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo na madaktari bingwa weneye weledi mkubwa, zamani upasuaji wa aina hii ulikua unafanywa nje ya taifa la Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: