Jengo la Alqamiy .. maandalizi ya kupokea mazuwaru yanaendelea

Maoni katika picha
Idara ya jengo la Alqami imetangaza kuwa maandalizi ya kupokea mazuwaru yanaendelea kipindi hiki cha karibu na ziara ya Arubaini.

Mkuu wa Majmaa Sayyid Niimah Alkhafaji amesema: “Watumishi wetu walianza maandalizi ya mwaka huu tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam, wameandaa kumbi na vyoo kwa ajili ya kutumiwa na mazuwaru, mwaka huu kutakua na mambo mbalimbali, kuna sehemu mpya zilizo pauliwa kwa ajili ya mazuwaru, sambamba na kuigawa Majmaa sehemu mbili, ya wanaume na wanawake”.

Idara ya Majmaa inatarajia kupokea watu elfu (30) kila siku wakati wa ziara ya Arubaini.

Alkhafaji akabainisha kuwa: “Majmaa hutoa huduma tofauti kwa mazuwaru, chakula milo mitatu pamoja na huduma zingine”.

Akasema: “Majmaa inatoa pia huduma ya afya kupitia vituo ambavyo huandaliwa kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala, ambayo imeshajipanga kutoa huduma hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: