Idara ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inajiandaa na ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya maonyesho ya Qur’ani kwenye barabara za (Yaa Hussein).
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali amesema “Watumishi wa Maahadi yetu wamekamilisha maandalizi ya kufanya maonyesho makubwa ya Qur’ani Jirani na nguzo namba (208), yatakayo husisha matawi tofauti, ikiwa ni pamoja na usomaji wa sura fupi za Qur’ani zikitanguliwa na surat Fat-ha, sambamba na kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani, mashindano ya kielimu na kupokea mazuwaru”.
Maahadi hufanya miradi tofauti na harakati mbalimbali zinazohusu Qur’ani tukufu kwa lengo la kuhimiza usomaji wa Qur’ani tukufu.
Akabainisha kuwa “Idara ya Maahadi imefanya vikao mara nyingi na viongozi wa ofisi za Maahadi, kwa ajili ya kubaini vipaombele vya maonyesho, kwani mwaka huu unatarajiwa kuwa na msongamano mkubwa wa mazuwaru baada ya kulegezwa masharti ya kujikinga na janga la Korona”.