Majmaa ya Qur’ani tukufu imejiandaa kufungua maukibu ya kiongozi wa wasomaji katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Majmaa ya Qur’ani tukufu kupitia miradi ya Qur’ani inajiandaa kufungua maukibu ya kiongozi wa wasomaji katika ziara ya Arubaini.

Mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’ani Sayyid Husseini Halo amesema: “Watumishi wa kituo wamekutana kujadili yanayo hitajiwa na maukibu kabla ya ufunguzi wake”, akasisitiza kuwa “Kuna umuhimu wa kufikia malengo kabla ya ufunguzi wa maukibu hiyo, kwa ajili ya kutumikia Ahlulbait (a.s) na mazuwaru wao”, akaashiria kuwa “Ni muhimu watu wa Qur’ani waishi katika mazingira ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) ili wawe katika watu wanaotumikia vizito viwili”.

Akafafanua kuwa “Kazi ya kujenga mabanda ya maukibu imeanza baada ya kubaini sehemu ya kila maukibu karibu na chuo kikuu cha Al-Ameed”.

Akaendelea kusema: “Zimepangwa shughuli muhimu zitakazofanywa katika maukibu na nyakati zake, maukibu zitaanza kutoa huduma mwanzoni mwa mwezi wa Safar”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: