Maahadi ya Qur’ani tukufu imekamilisha maandalizi ya mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Majmaa ya Qur’ani imekamilisha maandalizi yote yanayohusu kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru wa Arbainiyya.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Jawadu Nasrawi amesema “Mradi utaanzia katika mkoa wa Basra na kusambaa kwenye mikoa yote ya kusini na katikati hadi Karbala tukufu”.

Mradi huu ni sehemu ya kufundisha usomaji sahihi kwa mazuwaru na kuwatia moyo wale waliohifadhi kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

Akasema kuwa “Mradi wa kufundisha usomaji sahihi unavituo (70) vituo vinne katika hivyo tumeshirikiana na muungano wa vikundi vya Qur’ani vya Iraq”.

Akasisitiza kuwa “Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake ya mikoani imekua ikifanya mradi huu kwa mwaka wa kumi mfululizo kwenye ziara ya Arubaini na ziara zingine zinano hudhuriwa na mamilioni ya watu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: