Ujumbe kutoka Markazi Dirasaat Afriqiyya umetembelea wizara ya mambo ya nje ya Iraq na taasisi za kielimu kueleza harakati za Markazi katika bara la Afrika.
Mkuu wa Markazi chini ya kitengo cha Habari na utamaduni Shekhe Saadi Shimri amesema “Tumemuagiza Dokta Sarhani Ghulam Hussein muwakilishi wa Markazi Kwenda wizara ya mambo ya nje ya Iraq kukutana na viongozi na kueleza kazi zinazofanywa na Markazi katika bara la Afrika pamoja na familia za waafrika waishio Iraq”.
Akaongeza kuwa “Wamejadili namna ya kushirikiana katika kutekeleza miradi ya kibinaadamu na kitamaduni katika bara la Afrika” akasema “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Markazi Dirasaat Afribiyya kila mwaka hufanya mamia ya program zinazo lenga makundi tofauti ya waafrika”.
Ziara hiyo imelenga ofisi ya watumishi wa kigeni na idara zinazohudumia waafrika katika wizara ya mambo ya nje, aidha ujumbe huo umetembelea vyuo vikuu na taasisi za elimu na utamaduni.
Wamekubaliana kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutekeleza miradi mbalimbali, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa ujumbe huo Dokta Sarhani Ghulam. Akaongeza kuwa: “Lengo la ziara hiyo ni kuonyesha baadhi ya machapisho ya Markazi yanayo onyesha shughuli zinazofanywa na Markazi katika bara la Afrika, sambamba na kuandaa jamii inayofuata uislamu halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.