Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inajiandaa na ratiba ya hema za Qur’ani katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake inajiandaa kupokea mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini kupitia ratiba ya hema za Qur’ani.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema: “Maahadi imetumia uwezo wake wote katika kuandaa hema za Qur’ani zilizowekwa kwenye barabara zinazoelekea Karbala ambako watu wanaenda kufanya ziara ya Arubaini”.

Watumishi wa Maahadi wanafunga hema saba kwenye barabara inayoelekea Karbala, kuanzia mkoani Najafu, wilaya ya Hindiyya (Towareji) na mkoa wa Baabil na Waasitu”.

Akasema kuwa kazi kubwa itakayofanywa na kituo chetu ni kusahihisha usomaji wa Qur’ani tukufu, hususan surat Fat-ha, na usomaji wa Qur’ani kwa vikundi, mihadhara ya kifiqhi na kijamii, hali kadhalika Maahadi imeandaa jopo maalum kwa ajili ya kujibu maswali ya kisheria.

Akafafanua kuwa “Kutakua na mashindano kadhaa ya Qur’ani yakatayo endeshwa katika hema hizo, aidha kutakua na mashindano mbalimbali, kama vile mashindano ya kuandika, maswali na majibu na kuhifadhi Qur’ani tukufu”.

Akasema kuwa: “Maahadi itatoa zawadi za kutabaruku na vyeti kwa mazuwaru watakao fanya vizuri, kuna hema la bibi Ruqayya (a.s) maalum kwa watoto”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: