Kuendelea kwa vipengele vya program ya (Ashura ni njia ya ukamilifu wa familia)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia kinaendelea na program ya (Ashura ni njia ya ukamilifu wa familia), ilianza mwanzoni mwa mwezi wa Muharam na itaendelea hadi mwishoni mwa mwezi wa Safar.

Mkuu wa kituo bibi Sara Alkhafaar amesema “Hii ni moja ya program za kitamaduni zinazofanywa na kituo hiki, huendesha ratiba ya kufundisha malengo ya harakati ya Ashura kupitia mihadhara ya mada tofauti za kifamilia na zinginezo”.

Program inalenga wasichana wa mkoa wa Karbala.

Akabainisha kuwa: “Hutolewa mihadhara kwa lugha nyepesi inayo endana na aina ya walengwa, chini ya wahadhiri mahiri kutoka kituo cha uelekezaji, jambo ambalo hurahisisha ufundishaji wa maadili mazuri kwa wasichana na familia zao”.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kituo amesema: “Muitikio ulikua mkubwa, jambo hili ndio limetufanya tuongeze utoaji wa huduma na kuifikia jamii kubwa zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: