Kuanza kwa kituo cha kwanza cha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru katika mkoa wa Basra

Maoni katika picha
Asubuhi ya Alkhamisi kituo cha kwanza cha mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa mazuwaru wanaoenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini kimeanza kutoa huduma

Mradi huo unasimamiwa na kundi la wasomi wa Qur’ani kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia Maahadi za Qur’ani zilizopo mikoani.

Kituo cha kwanza mwaka huu kimefunguliwa katika mkoa wa Basra kwa kushirikiana na muungano wa wasomaji wa Qur’ani katika mkoa huo, chini ya umoja wa vikundi na taasisi za Qur’ani za Iraq, nacho ni kimoja kati ya vituo vinne vinavyo endeshwa kwa kushirikiana na umoja wa wasomaji wa Qur’ani.

Mradi huo unahusisha ufundishaji wa surat Fat-ha na sura fupi, pamoja na nyeradi za swala, vikao vya usomaji wa Qur’ani ambavyo watashiriki waliohifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, sambamba na kufanya mashindano ya usomaji wa Qur’ani kwa mazuwaru wanaoenda kwa bwana wa mashahidi (a.s).

Mradi unavituo (70) katika mkoa wa Karbala na mikoa mingine, wanafuata utaratibu mmoja, na umekua ukifanyika kwa muda wa miaka kumi mfululizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: