Wataalamu wa Alkafeel wanatoa elimu ya uokozi na huduma ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Ahlulbait (a.s)

Maoni katika picha
Wataalamu wa Alkafeel wanatoa huduma ya uokozi na huduma ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Ahlulbait (a.s) katika kujiandaa na ziara ya Arubaini.

Mkufunzi Sayyid Sefu Nasrullah amesema “Semina itakua ya siku mbili, sehemu ya kwanza imepewa jina la (Katika kila nyumba muokozi) wamefundishwa mbinu za kuokoa majeruhi na watu wenye matatizo ya moyo”.

Akaongeza kuwa “Sehemu ya pili imepewa jina la (Huduma ya kwanza) wamefundishwa namna ya kusaidia mtu aliyevunjika mfupa na mwenye tatizo la ubongo”.

Akabainisha kuwa “Semina imelenga wanafunzi wa udaktari kutoka kitivo cha udaktari na afya ya meno”.

Kwa mujibu wa Nasrullah “Semina hii ni sehemu ya kujiandaa kutoa huduma kwa mazuwaru wa baba wa watu huru na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: