Ujumbe kutoka Markazi Dirasaat Afriqiyya umetembelea chuo kikuu cha Faluja kujadili ushirikiano katika mambo yanayo husu Afrika [b/].
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Ziara hiyo inalenga kutambulisha harakati za Markazi katika bara la Afrika na jinsi inavyo hudumia familia za waafrika waishio Iraq, sambamba na kujadili namna ya kushirikiana katika makongamano na warsha za kielimu”.
Mkuu wa ujumbe huo Dokta Sarhani Ghulam Hussein amesema “Uongozi wa chuo kikuu cha Faluja na wakufunzi wake, wamepongeza kazi zinazofanywa na Markazi katika bara la Afrika na wamekubali kutoa ushirikiano”.
Akabainisha kuwa “Markazi imekabidhi nakala ya machapisho yake na machapisho kutoka kitivo cha masomo ya kiislamu na kanuni”.