Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya) zinatoa wito kwa waumini kuhudhuria hafla ya kupandisha bendera ya kuomboleza Imamu Hassan (a.s) siku ya Jumamosi mwezi saba (7) Safar, ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kifo chake (a.s), bendera hiyo itapandishwa katika Ataba tajwa baada ya swala ya Magharibi.