Nadwa ya wasichana kuhusu uwelewa wa kiitikadi katika maneno ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imefanya nadwa kuhusu uwelewa muhimu na madhumuni ya kiitikadi katika maneno ya bibi Zainabu binti Ali (a.s).

Mkuu wa Maahadi hiyo bibi Manaar Aljaburi amesema: “Nadwa imehusisha usomaji wa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Hauraa Salim, kisha ukatolewa mhadhara na Dokta Inasi Darughi kutoka chuo kikuu cha Alkafeel, ameongea visa vya namna ya kumtambua muumbaji na mifano mbalimbali, kwa kutumia aya za Qur’ani tukufu na maneno ya bibi Zainabu (a.s) katika mapambano yake na waovu wa bani Umayya”.

Kwa mujibu wa Jaburi hakika Maahadi inafanya juhudi kubwa ya kuendesha vikao kama hivi na kusambaza ujumbe kwa waumini.

Mkuu wa Maahadi akabainisha kuwa “Nadwa imepata muitikio mkubwa, washiriki wamechangia mada na kuuliza maswali mengi hususan yanayohusu tauhidi na kumtambua Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: