Kitengo cha Dini kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini kimetangaza kukamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini, mwaka huu tunatarajia kuwa na idadi kubwa ya mazuwaru tofauti na miaka ya nyuma.

Rais wa kitengo cha Dini Shekhe Swalahu Karbalai amesema “Kitengo kimeandaa harakati za pekee, ikiwa ni pamoja na machapisho ambayo baadhi yake yameandikwa kwa lugha za kigeni, ambazo ni lugha ya Kiurdu, Kiengereza na Kifaransa.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeongeza idadi ya mubalighina na vituo vya Tablighi, hususan kwenye barabara ya (Najafu – Karbala) inayo pitia kwenye mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye malango ya kuingia katika mji mtukufu wa Karbala”.

Kuhusu kupokea wahudumu wa kujitolea amesema kuwa “Kitengo kimepokea idadi kubwa ya wahudumu wa kujitolea wakiwemo mashekhe kutoka nje ya nchi, wanaingizwa kwenye mradi wa Tablighi kwa kuzingatia adabu za ziara, idadi kubwa wanatoka mkoa wa Bagdad, wanajitolea kutekeleza jukumu hili adhim la kuamrisha mema na kukataza mabaya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: