Kitengo cha utumishi kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini, kikiwa na wahudumu wa kujitolea zaidi ya elfu mbili.

Makamo rais wa kitengo Mhandisi Abbasi Ali amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), wameandaa sardabu za haram tukufu kwa kuzisafisha na kuweka mahitaji yoto ya lazima kwa watumishi wakati huu wa ziara tukufu”.

Akaongeza kuwa “Tumeandaa sehemu nne za kutunzia mabeji ya wageni pamoja na kufungua sehemu tatu mpya za kutunzia viatu” akasema “Tumeandaa deli elfu (50) za maji na vipande vya barafu elfu nne, kwa ajili ya kugawa kwa mazuwaru na mawakibu za kutoa huduma”.

Kuhusu sehemu za kulala wahudumu wa kujitolea amesema kuwa “Kitengo kimeandaa baadhi ya shule na kuweka mahitaji ya lazima kwa ajili ya malazi ya watu wakati wa ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: