Zaidi ya vitambulisho elfu saba vimetolewa kwa wakuu wa mawakibu zitakazo shiriki kwenye ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu, kimetoa zaidi ya vitambulisho (7000) kwa wakuu wa mawakibu Husseiniyya, ili kurahisisha kuingia katika mji wa Karbala kufanya ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyasiriy amesema “Watumishi wa kitengo wamekamilisha usajili wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyo kuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini, tumetoa zaidi ya vitambulisho elfu (7000) kwa mawakibu zilizo sajiliwa rasmi”.

Kuhusu utendaji wa kazi amesema kuwa “Kitengo huangalia vipaombele vya maukibu, kisha taarifa za maukibu hiyo hupelekwa ofisi ya palisi wa Karbala na kikosi cha haramaini tukufu kwa ajili ya kupewa ruhusa ya kuingia katika mji wa Karbala”.

Mkuu wa polisi wa Karbala Brigadier General Qasim Muhammad amesema “Idara yetu inafanya kazi ya kurahisisha uingiaji wa Mawakibu Husseiniyya kwenye vizuwizi vya nje, hususan mawakibu za kigeni zinazokuja kutoka Jamhuri ya Iran, Adharbaijan, Sirya na baadhi ya nchi za kiarabu kwa kufuata taratibu za kisheria”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: