Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Ruqayya (a.s) kwa ushiriki wa wanafunzi wa kike.
Kiongozi wa Maahadi hiyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu bibi Manaar Aljaburi amesema “Maahadi imefanya majlisi iliyo hudhuriwa na wanafunzi wa kike, kwa lengo la kumtambulisha bibi huyo kibenzi kwa Imamu Hussein (a.s), na kuwapa nafasi ya kuomboleza msiba wa Ahlulbait (a.s)”.
Maahadi inafanya kazi ya kulea vipaji vya wanafunzi kupitia shughuli zinazo fungamana na watu wa nyumba ya Mtume, majlisi hiyo imepambwa na picha zilizochorwa na wanafunzi na kazi zingine za mikono, zenye mafungamano na Ahlulbait (a.s) na malalo zao takatifu, kazi hizo zinaonyesha mapenzi yao kwa Qur’ani na watu wa nyumba ya Mtume watakasifu.