Ugeni wa madaktari kutoka chuo cha Malkia Landan umetembelea chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Ugeni wa madaktari kutoka chuo cha Malkia Landan – umetembelea Iraq na kufika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ugeni huo unaongozwa na Dokta Hilali Safaar, umekutana na makamo rais Dokta Maitham Hamiid Qambar, na Mkuu wa kitivo cha udaktari Dokta Rahim Mahadi pamoja na wakufunzi kutoka vitengo vingine.

Wamejadili namna ya kushirikiana na kubadilishana uzowefu, sambamba na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya afya hapa Iraq.

Ugeni umetoa mhadhara kwa wanafunzi na wakufunzi wa chuo kuhusu mfumo mpya na mbunu za ufundishaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: