Mradi wa majengo ya viwanda na maabara ya Atabatu Abbasiyya umepiga hatua kubwa

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi kinaendelea na hatua ya pili ya ujenzi wa majengo ya viwanda na maabara za Atabatu Abbasiyya.

Mhandisi mkazi Murtadha Habibu Hashim amesema “Hatua ya pili ya mradi inahusisha ujenzi wa majengo Matano ya ghorofa mbili na magodauni”.

Akaongeza kuwa “Ukubwa wa kila ghorofa ni mita za mraba elfu tatu na kila godauni linaukubwa wa (mita za mraba 2500), eneo lote kwa ujumla linaukubwa wa dunam (63) sawa na mita za mraba (160,000)”.

Kwa mujibu wa Hashim “Kazi inaendelea ya kuweka bomba za maji, kujenga sehemu za ofisi na maeneo mengine”, akasema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili ijayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: