Idara ya teknolojia ya mitandao katika kitengo cha Habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya ziara ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa niaba, katika kumbukizi ya kifo chake Jirani na kaburi lake huko Baqii katika mji wa Madina.
Kila anaependa kufanyiwa ziara ajisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel kwa kutumia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/
Aidha unaweza kutumia App inayopatikana kwenye simu ganja za kisasa (smart phone): https://alkafeel.net/Apps/Arabic/
Kwa mujibu wa idara hiyo, ziara itafanywa na waumini wa kujitolea wanaoishi Madina, watafanya ziara maalum na swala ya rakaa mbili kwa nia ya kukidhi haja na kufanya mambo yawe mepesi.