Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Jumamosi sawa na tarehe (6 Safar 1444h) imepandisha bendera ya Imamu Hassan (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, sambamba na kupandishwa bendera hiyo kwenye Ataba zote, kama ishara ya kuhuisha utiifu kwa Ahlulbait (a.s).
Hafla ya kupandisha bendera imefanyika karibu na mlango wa Imamu Hassan (a.s), kwenye eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Hafla hiyo imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustafa Murtadha Dhiyaau-Dini, naibu wake, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo, baadhi ya viongozi wa Dini na kundi la waumini, hafla imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Haidari Jalukhani kisha ikasomwa ziara ya Imamu Hassan (a.s) na Sayyid Ali Amiin Mamitha, halafu ikasomwa kaswida na mshairi fasaha Ali Safaar Karbalai.
Kisha wahudhuriaji wakaelekea kwenye upandishaji wa bendera ya Imamu Hassan (a.s), iliyoshonwa na kudariziwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Halafu ukafuata mhadhara wa kuomboleza uliotolewa na Sayyid Hashim Batwaat, majlis ikahitimishwa kwa mashairi ya kuomboleza yaliyosomwa na Qahtwani Albudairi.
Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya na Abbasiyya) zilikua zimesha toa wito kwa waumini wote wahudhurie hafla za upandishaji wa bendera ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan (a.s) jioni ya leo -mwezi saba Safar- siku aliyo uawa kishahidi Imamu Hassan (a.s).