Kitengo cha Dini kimeshiriki kwenye kongamano la kumi na moja la mubalighina wa ziara ya Imamu Hussein (a.s) ya Arubaini, lililo andaliwa na hauza ndani ya ukumbi wa jengo la Alawiyya katika mji wa Najafu.
Kitengo kimewakilishwa na makamo rais wake Shekhe Aadil Wakiil, amesema: “Kongamano limefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ziara ya Arubaini ni mfumo wa Shia katika utiifu na utekelezaji), limehudhuriwa na kundi la walimu wa hauza na viongozi wa mji wa Najafu pamoja na mamia ya mubalighina”.
Kongamano hilo limehutubiwa na Mheshimiwa Riyaadh Hakiim, amebainisha kuwa “Ziara ya Arubaini inamambo mengi, huzingatiwa ni sehemu ya kujali mhanga wa Imamu Hussein (a.s) na kuhuisha misingi ya uislamu”.
Akafafanua kuwa “Ziara inakumbusha yaliyowatokea Ahlulbait (a.s), sambamba na kuonyesha majukumu ya mubalighina na ulazima wa kujibu shubha na kuonyesha umaalum wa ziara hii”.
Hauza ya Najafu huweka mubalighina kwenye kila njia inayoelekea Karbala, hususan zinazotumiwa na mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wanaotembea kwa miguu, Atabatu Abbasiyya inamchango mkubwa katika swala hilo, sambamba na kushiriki kwenye ratiba hiyo kupitia mubalighina wake watukufu.