Chuo kikuu Alkafeel kinaomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel leo siku ya Jumapili kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Majlisi imehudhuriwa na rais wa chuo hicho Dokta Nuris Dahani, idara za chuo, wakufunzi na wanafunzi.

Imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Ahmadi Zamiliy, kutoka Maahadi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tawi la Najafu.

Kisha akapanda kwenye mimbari Mheshimiwa Sayyid Jafari Murawwiji, ameongea mambo mbalimbali kuhusu historia ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s), akaangazia “Juhudi za Imamu katika kuokoa ukhalifa na kulinda damu za waislamu, na kuzuwia umma usiharibike”, akasisitiza kuwa “Alijitoa katika kufundisha wafuasi wake Dini sahihi na utamaduni wa uislamu halisi uliofundishwa na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: