Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanahuisha kumbukumbu ya kifo cha mkarimu wa Ahlulbait (a.s)

Maoni katika picha
Jioni ya Jumapili mwezi (7 Safar 1444h) maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya imefanya matembezi ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kumbukumbu ya kufa kwa Mkarim wa Ahlulbait Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Matembezi hayo yametanguliwa na jeneza la kuigiza na yalianzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Wakati wa matembezi hayo waombolezaji wamesoma kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni ya msiba huu mkubwa.

Maukibu ilipofika kwenye haram ya bwana wa mashahidi (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza ambapo kaswida na tenzi mbalimbali zimesomwa, zilizo eleza dhulma aliyofanyiwa Imamu Hassan (a.s) na watawala wa zama zake, hadi akuuawa kwa sumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: