Kitengo cha kusimamia haram kimeingiza gari za wagonjwa na utoaji wa huduma ya kwanza katika haram wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha kusimamia haram tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimeingiza gari (7) mpya za wagonjwa na huduma ya kwanza katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini.

Kiongozi wa idara ya kubeba mazuwaru Sayyid Hasanaini Ali amesema kuwa “Kitengo kimeandaa gari saba mpya kwa ajili ya kutoa huduma ya uokozi, zitawekwa katika vituo vya katikati ya mji na eneo la karibu na malalo mbili takatifu, aidha kuna gari zingine kumi kwa ajili ya kubeba mazulia na vitu vingine, gari hizo zipo katika jengo la Alqami, Ummul-Banina na sehemu zingine”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wa kitengo wanazamu tatu kwa siku, yaani wanafanya kazi muda wote usiku na mchana, wanasaidia kubeba wazee na watu wenye ulemavu wanaowasiri Karbala kufanya ziara ya Arubaini”.

Akabainisha kuwa “Gari zinafanyiwa matengenezo na watumishi wa kitengo muda wote, zipo tayali kubeba watu wakati wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: