Chuo kikuu cha Alkafeel kimekamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na kuwahudumia.

Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani amesema “Chuo kitakua na maukibu mbili za kutoa huduma, moja itakuwa kwenye barabara ya (Najafu / Karbala) karibu na nguzo ya (23) na nyingine katika mji wa Kufa karibu na malalo ya swahaba mtukufu Maitham Tamaar (a.s), zinamahitaji yote muhimu kwa ajili ya mazuwaru watukufu”.

Akaongeza kuwa “Chuo kimekua kikihudumia mazuwaru kwa mwaka wa kumi mfululizo, hugawa chakula, vinywaji, huandaa sehemu za kulala kwa wanaume na wanawake sambamba na kuwepo kwa wanachuoni wanaojibu maswali ya kisheria, kupitia mradi wa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu”.

Akaendelea kusema “Maukibu za chuo hutoa huduma za afya pia pamoja na huduma ya kuelekeza waliopotea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: