Kitengo cha usafiri kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha maandalizi ya ziara tukufu ya Arubaini.

Rais wa kitengo cha usafiri Sayyid Abduljawaad Kaadhim amesema “Tumeandaa gari za aina na ukubwa tofauti, zikiwemo gari za wagonjwa na utoaji wa huduma za afya, kwa lengo la kusaidia kusafirisha mazuwaru na kuwafikisha salama katika mji wa Karbala kwa ajili ya kufanya ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa “Watumishi wetu mwaka huu wamekamilisha maandalizi mapema, sambamba na kuzingatia idadi ya mazuwaru wanaotarajiwa kuja mwaka huu, tambua kuwa gari zetu tumezifanyia matengenezo makubwa”.

Akaendelea kusema “Kuna gari zimeandaliwa kwa ajili ya kutoa huduma maalum”, akafafanua kuwa “Tumeandaa gari maaluma la kubeba mafundi ambao wako tayali kutengeneza gari lolote litakalo haribika wakati wa kazi”.

Akasisitiza kuwa “Watumishi wetu wanafanya kazi saa (24) wanazamu tatu, wanasaidiwa na watoa huduma wa kujitolea ambao huja kila mwaka, aidha tumeongeza gari kutoka kwa watu tofauti wanaojitolea gari zao kuja kusaidia kubeba mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: