Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya semina kwa wanafunzi wake wanaojitolea kutoa huduma kwenye vituo vya afya

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya semina elekezi kwa wanafunzi wake wanaojitolea kutoa huduma kwenye vituo vya afya kupitia maukibu ya Ummul-Banina (a.s) iliyopo kwenye barabara ya Najafu – Karbala.

Mkufunzi wa semina hiyo alikua ni Dokta Ridhwa Muhammad, ameeleza mbinu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya kwa mazuwaru, na utoaji wa huduma za uokozi kwa mazuwaru.

Upande wa taaluma wameongea wahadhiri wauguzi kutoka chuo kikuu ambao ni (Muhammad Baaqir, Islamu Maajid na Ali Alaa Mahmuud), wameeleza misingi ya kibinaadamu katika utoaji wa huduma za uokozi wa majeruhi na wahanga wa majanga.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: