Usomaji wa Qur’ani katika mji wa Muthanna kwenye mradi wa kujifunza usomaji sahihi kwa Mazuwaru

Maoni katika picha
Kimefanyika kikao cha usomaji wa Qur’ani katika mkoa wa Muthanna kupitia mradi wa kujifunza usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru unaofanywa na Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa shekhe Jawadi Nasraqi amesema “Kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika vituo vya ufundishaji wa usomaji sahihi kunalenga kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii na kwa mazuwaru wa Bwana wa Mashahidi (a.s) nalo ni jambo muhimu katika kuhakikisha unapatikana utumishi wa vizito viwili”.

Akaongeza kuwa “Kundi la wasomaji mahiri wameshiriki kwenye kikao hicho pamoja na mazuwaru wanaoenda Karbala”, akasema “Hakika vituo vya kufundisha usomaji wa Qur’ani vimewekwa kwenye mikoa tofauti”.

Mradi unalenga kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha Surat Fat-ha na baadhi ya sura fupi zinazo somwa mara nyingi wakati wa swala, kunamashindano ya kielimu pia, mradi huu unajumla ya vituo (75) kuanzia kusini ya Iraq hadi Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: